|
||||||||||||||||||||||
Watazamaji wa Kenya wasifu Gongfu ya China
(GMT+08:00) 2009-06-02 19:36:01
Wachezaji nyota wa Gongfu wa
China Bruce Lee na Jackie Chan wanajulikana sasa kote barani Afrika,
hata kila mtu anaweza kuiga kidogo vitendo vyao kama walivyofanya kwenye
filamu zao. Hivi karibuni shirikisho la mchezo wa Wushu la China
lilituma ujumbe wa watu 28 kufanya maonesho ya michezo ya Gongfu barani
Afrika, maonesho hayo yamewavutia watazamaji wengi wa Afrika. Tarehe 27
usiku ujumbe huo ulifanya maonesho murua katika kituo cha mkutano cha
kimataifa cha Kenyatta huko Nairobi, Kenya. Maonesho hayo yaliwafanya
watazamaji wafurahi sana na kupiga makofi mara kwa mara.
Safari hii ujumbe huo wa Wushu wa China utafanya ziara katika nchi tano, yaani Gabon, Kenya, Zambia, Malawi na Tanzania. Ziara hiyo itaonesha utamaduni wa Wushu wa China kwa watu wa Afrika, ili kuwawezesha wananchi wa Afrika waongeze ufahamu wao kuhusu China na kuhimiza mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Afrika. Naibu mwenyekiti wa shirikisho la mchezo wa wushu la China Bw. He Qinglong alisema:
"watu wa Kenya wanapata ufahamu kuhusu Wushu ya China kwa njia ya filamu za Gongfu, wanawajua Jet Li na Jackie Chan. Tunataka kueneza utamaduni wa Wushu kwa watu wa Afrika kwa kupitia shughuli hizo. Tunapenda kujenga daraja la urafiki kati ya China na Afrika, kati ya watu wa China na wa Kenya kwa njia ya Wushu."
Baada ya maonesho hayo kumalizika, kocha mmoja wa Wushu wa atabaki nchini humo na kutoa mihadhara na mafunzo ya muda mfupi kwa vijana wa Kenya wanaopenda Wushu, ili kuwewezesha waongeze ufahamu wao kuhusu utamaduni wa Wushu wa China. Na kwa wachezaji wa Wushu wa China, hii pia ni mara yao ya kwanza kufanya maonesho barani Afrika, wanaona furaha na fahari sana. Bw. Lu Jie kutoka mkoa wa Anhui alisema:
"nilianza kujifunza Wushu nilipokuwa na umri wa miaka 11 hadi 12, na nimefanya mazoezi kwa miaka 12. Naona fahari sana kwamba Wushu ya China ina historia ndefu tangu enzi na dahari. Maonesho hayo si kama tu yameonesha mambo mazuri ya nchi yetu, bali pia yanaweza kuhimiza mawasiliano kati ya watu wa nchi mbili."
Baadhi ya watazamaji wanaonesha hamu kubwa juu ya utamaduni wa Wushu ya China baada ya kutazama maonesho hayo. Kati yao mwanafunzi mmoja anayeitwa Kennedy ambaye anasoma kwenye chuo cha Confucious katika chuo kikuu cha Nairobi cha Kenya, na anapenda kucheza Taijiquan baada ya masomo. Bw. Kennedy alisema, maonesho hayo yamemfumbua macho, pia yameongeza zaidi hamu yake ya kujifunza utamaduni wa China, alisema:
"naona maonesho ya leo yanavutia sana. Nina matumaini kuwa iko siku nitacheza Gongfu vizuri kama wachezao hao wa China, nitajitahidi kufanya mazoezi. Lakini baadhi ya vitendo vinahitaji unyumbufu wa miwili, wala si rahisi kuvifanya vizuri. Wushu si kama tu ni ustadi wa kujilinda, bali pia inaweza kujenga afya na kuondoa magonjwa, mbali na hayo, Wushu pia inaweza kuhimiza mawasiliano ya kiutamaduni kati ya nchi mbalimbali, tunajifunza mambo mengi kutokana na Wushu."
Safari hii pia ni mara ya kwanza kwa Mkuu wa kundi la Kayamba Afrika linayojulikana sana nchini Kenya Bw. Juma Odemba kutazama maonesho mazuri ya Wushu kama hayo. Alisema:
"naona maonesho ya leo yanavutia sana, ni ajabu ya kushangaza. Hii ni mara yangu ya kwanza kutazama mwenyewe maonesho ya Wushu, zamani nilitazama kwenye televisheni, sasa nayaona kwa macho yangu, kweli yanasisimia sana."
Naye waziri wa utamaduni na urithi wa taifa wa Kenya Bw. William Ole Ntimama pia alitazama maonesho hayo. Alisifu sana maonesho mazuri ya wachezaji wa China, na kusema kuwa China na Kenya ni marafiki wakubwa, nchi hizo mbili zitapanua ushirikiano katika mambo ya utamaduni na kuimarisha maelewano na urafiki kati ya wananchi wa nchi hizo mbili. Bw. Ntimama alisema:
"China ni rafiki mkubwa zaidi wa Kenya. China ilitambua uhuru wa Kenya na kuanzisha uhusiano wa kibalozi na nchi yetu muda mfupi tu baada ya Kenya kujipatia uhuru. Historia ya Kenya inafanana na ile ya China, zote zilipambana na uvamizi wa wakoloni na kupigania uhuru wa taifa. Tulituma vijana hodari kwenda kusoma nchini China, na wengi wao wamekuwa wataalamu hodari baada ya kurudi. Ni matumaini yangu kuwa China na Kenya zinaweza kuimarisha mawasiliano katika mambo ya utamaduni, na mchezo wa Wushu ni kama chombo kimoja kizuri cha kiutamaduni, wakati kinapoleta furaha kwa watu, hasa vijana wa Kenya pia tunaweza kujifunza mambo mengi kutoka kwake."

No comments:
Post a Comment