Thursday, October 8, 2015

MAKAMU WA RAIS GHALIBU BILALI ANATARAJIWA KUWA MWENYEJI WA MATEMBEZI YA SARATANI

Timothy Marko.Makamu wa rais Dk Ghalibu Bilali anatatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika matembezi ya hisani yakuchangia gharama za Wahanga wa saratani ya Kizazi yanayotarajiwa kufanyika Jijini Dar es salam mapema mwezi huu.
Kwamujibu wataarifa iliyotolewa na Taasisi yautafiti wa magonjwa ya Binadamu NIRM Mapema hii leo ilieleza kuwa ,matembezi hayo yanalenga ukusanyaji wa fedha kwajiili yakuchangia wahanga wa ugonjwa wa saratani ya shingo yakizazi wapatao 48000 Kwa mwaka .
''Takwimu zinaonesha kuwa katika kipindi mwaka 2002 jumla yawagonjwa milioni 14 wagonjwa 48000 hugundulika kuwa nasaratani yashingo yakizazi ambapo wagonjwa nane hufariki kutokana ugonjwa wa saratani ya kizazi ''Ili eleza taarifa hiyo .
Aidha Taarifa hiyo ilieleza kuwa ugonjwa wa saratani ya kizazi ni yapili wakati huohuo sararatani ya matiti ikiongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi ambapo wengi wawagonjwa hao ni wanawake .
Katika hatua nyingine,ripoti hiyo ili eleza kuwa katika ukanda wa afrika mashariki nchi ya Rwanda imekuwa ikitoa chanjo ya saratani ya matiti kwa asilimi 33 na kusitiza kuwa ugonjwa wa saratani unasababishwa nakirusi cha Hypatasis.